Wahitimu wa jeshi la akiba wilaya ya hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufuata na kuzingatita kiapo walichokiapa na kuwa wazalendo ,watiifu na kufuata maadali waliyoyapata darasani wakati wa mafunzo hayo.
Akifunga mafunzo hayo katika shule ya msingi lyamungo ari kijiji cha wari sinde mkuu wa wilaya ya hai Juma Said Irando amesema mbali na mafunzo hayo waliyoyapata pia yapo waliyofundishwa kuwa wazalendo,ukomavu ujasiri uhodari na utaifa wa kulitetea taifa lao.
Irando amewataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri katika jamii na kuwa mfano bora kwa kutojiingiza kwenye ulevi wa kupindukia,matumizi ya madawa ya kulevia,vitendo vya rushwa na kutoa siri mbalimbali za taifa.
Aidha Irando amempongeza James Mushi ambaye ni diwani wa kata ya machame kwa kuwa mmoja walionyesha uzalendo kwa kuudhuria mafunzo na kuhitimu kwani ni mfano bora kwa kiongozi na kwa jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Gwamaka Ngondya mshauri wa jeshi la akiba wilaya ya hai amesema katika mafunzo hayo wahitimu walifundishwa silaa,kwata,huduma ya kwanza,usomaji wa ramani,mbinu za kivita,ujanja wa porini,utimamu wa mwili,uchimbaji wa maandaki na mabomu ya kurusha kwa mikono.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai