Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai limemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuwasimamia watendaji wa vijiji na Kata katika kuhamasisha wananchi kutunza mazingira kwa kuotesha miti maeneo yanayozunguka vyanzo vya maji.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Edmund Rutaraka amtoa kauli hiyo katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 ambapo alisisitiza kuwa maeneo mengi ya vyanzo vya maji yanahitaji uboreshaji wa haraka kwa kupanda miti.
"Maeneo mengi ya vyanzo vya maji yameharibika hususani kingo za maeneo hayo kutokana na wananchi kulima ndani ya mito jambo ambalo ni hatari kwa vyanzo hivyo Mkurugenzi lazima ulisimamie kwa umakini" Alisema Rutaraka.
Hatua ya baraza hilo iimekuja baada ya Kamati ndogo ya kufuatilia halia ya uharibifu wa mazingira iliyoundwa katika baraza la robo ya pili kuwasilisha taarifa yake iliyoonesha kuwepo kwa uharibifu wa mazingira katika vyanzo vingi vyamjai vinavyohusisha ukataji miti na baadhi ya wananchi kulima katika vyanzo hivyo.
Awali akitoa taarifa za kamati hiyo Nasibu Mndeme amesema maeneo ya vyanzo vya maji yamevamiwa na kufanyika shughuli mbalimbali zikiwemo kilimo cha mboga mboga, vilevile ukataji wa miti kwa ajili ya Mbao.
"Mhe. Mwenyekiti baadhi ya maeneo yamevamiwa sana na watu jambo ambalo linapelekea upungufu mkubwa wa maji na hata magonjwa ya mlipuko kutokana na baadhi ya watu kutumia sehemu za mito kwa kutengenezea pombe haramu yagongo na kumwaga mabaki ndani ya maji ambayo hutumiwa na binadamu".
Hata hivyo kamati ndogo imetoa pendekezo kwa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anapanda miti na kuitunza ili iweze kukuwa pamoja na kutunza mazingira ya vyanzo vya maji ili viweze kuwa endelevu katika kutoa huduma kwa wananchi
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai