Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro Juma Irando amekabidhi rasmi kwa mkuu mpya wa wilaya hiyo Amiri Mkalipa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Hai na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.
Irando amewashukuru watumishi wa umma katika wilaya ya Hai pamoja na ofisi ya Chama Cha Mapinduzi wilayani humo kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika utekelezaji wa majukumu yake na kuwaomba waendeleze ushirikiano huo kwa mkuu wa wilaya wa sasa Amiri Mkalipa.
Irando amehamishwa wilaya ya Hai na kwenda kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mkuu wa wilaya ya Hai Amiri Mkalipa ameeleza kuwa ataanzia pale alipoishia Irando huku akimpongeza kwa kumaliza mgogoro wa KIA na wananchi waliovamia eneo la uwanja huo na kufukuta kwa muda mrefu.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai