Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya wila ya Hai imemtaka mkandarasi anayejenga kituo cha afya Nkwansira kutoa milango yote iliyowekwa kwenye kituo hicho na kuweka milango yenye ubora pamoja na kufuata maelekezo ya mhandisi wa wilaya.
Kamati hiyo pia imemtaka Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha kuwa mapungufu yaliyoonekana kwenye mradi huo hasa milango iliyowekwa kinyume na maelekezo ya Mhandisi wa ujenzi inaondolewa na kuwekwa milango yenye ubora na kwakutumia mbao imara.
Akizungumza katika ziara hiyo makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Swalehe Kombo amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anamshirikisha na kufuata maelekezo ya mhandsi wa ujenzi wa wilaya katika kila hatua ili kuepuka hasara inayoweza kujitokeza.
“tumegundua kuwa mkandarasi alichokifanya ameweka milango kabla ya ushauri wa mhandisi ,kwa wakati mwingine msianzishe kitu kabla ya mhandisi kushauri ili kuzuia hasara inayojitokeza maana mhandisi ameshauri hii milango haifai pamoja na mbao zilizotumika hazifai, hivyo ni vema pawepo na ushirikishwaji kati ya pande hizi mbili” aliongeza Swalehe.
Kwa upande mwingine mkandarasi huyo ameiomba kuongezewa muda ili aweze kukamilisha ujenzi huo ambao amebakiza ujenzi wa kichomea taka na kuweka sinki ,ombi ambalo lilikubaliwa na kamati hiyo iliyomtaka kufuata taratibu zote za kuongeza muda na kuahidi kurudi kukagua ujenzi huo kabla ya kukabidhiwa kwa mradi huo.
Kituo cha afya Nkwansira kinajengwa na fedha za tozo ya miamala ya simu shilingi 250,000,000/= na kinatarajiwa kutoa huduma kwa wakazi wa Kata ya Masama Magharibi.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai