Kamati ya fedha uongozi na mipango wilaya ya Hai imefanya ziara katika kata mbali mbali za wilaya hiyo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na Uvico 19.
Miradi iliyotembelewa ni ile ya Afya na Elimu ambayo imetekelezwa kupitia fedha hizo zilizotolewa na Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa miradi hiyo, Afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Erick Marishamu amesema kuwa mpaka sasa wanafunzi wengi katika wilaya hiyo wamesharipoti shuleni kupitia utaratibu uliowekwa na Serikali.
“Sehemu kubwa yah ii miradi inalenga sekta ya elimu na afya na fedha nyingi ni zile zinazotokana na IMF maarufu kama fedha za Uvico 19 ambazo zimesaidia sana Halmashauri yetu katika mapokezi ya watoto wa kidato cha kwanza, kwahiyo hii ziara ni ya kawaida ambayo kamati ya fedha uobgozi na mipango huwa inafanya kila robo mwaka”
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bomang’ombe Evod Njau amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan kwa kuwapatia fedha hizo zilizotekeleza miradi ya elimu na Afya kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ilipokea jumla ya shilingi milioni 860 kutoka Serikalini kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 43 vya madarasa ambavyo vimeshakamilika na wanafunzi kuripoti shuleni.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai