Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Hai imewataka wakandarasi pamoja na mafundi kukamilisha miradi wanayoisimamia kwa wakati ili kuweza kuwafikia Wanufaika.
Kamati hiyo imetoa maelekezo hayo wakati wa na Mwenyekiti wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika shule za Mukwasa,Hai,Bomang'ombe,Kware na Kibaoni pamoja na Zahanati ya Elerai.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Hai,ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Edmund Rutaraka amesema Wakandarasi kutokamilisha miradi kama ilivyo kusudiwa inawanyima wananchi haki ya kupata huduma Kama ilivyokusudiwa.
Kwa upande mwingine amewapongeza viongozi wa serikali za vijiji ,wakuu wa shule pamoja na wanachi kwa ujumla kwa kuweza kujitokeza na kushiriki na kusimamia shughuli mbali mbali katika ujenzi wa miradi hiyo miradi na kutatua baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake.
Aidha Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amewataka wananchi kuendelea kushiriki katika ujenzi wa miradi hiyo ili kusaidia usalama wa vifaa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai