KAMATI ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro imesema kuwa imeridhika na hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayyotekelezwa na halmashauri ya Wilaya ya Hai
Kauli hiyo inatolewa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoani Kilimanjaro, Patrick Boisafi baada ya kutembelea miradi sita ya kimaendeleo ikiwemo ya elimu , afya na miundombinu ya barabara
Boisafi amesema kuwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 /2020 katika wilaya ya Hai umelekelezwa kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyostahili kutokana naushirikiano na usimamizi mzuri wa wataalamu pamoja na viongozi wa Chama hicho ngazi ya wilaya.
Akiwa katika mradi wa shule ya Sekondari ya Tambarare iliyoanzaa kupokea wanafunzi mwaka huu amesa kuwa uanzishwaji wa shule hiyo umesaidia kuboresha elimu kwa wanafunzi wanaofauli kuingia kidato cha kwanza ambao walikuwa wanatembea umbali wa kilometa 24 kwenda na kurudi hadi shule ya sekondari ya KIA
Mwenyekiti huyo amesema kupatikana kwa usajili wa shule hiyo litapunguzi adha watoto wa vijiji vya Mtakuja na Tindigani kwenda mwendo mrefu kufuata elimu na pia uanzishwaji huo utasaidia kupunguza tatizo la mimba za utoto kwa wanafunzi wa maeneo hayo
Boisafi amesema kuwa halmashauri imeweza kutoa fedha za makusanyo ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye walemavu ambapo ni agizo la serikali la kila halmashauri kutenga fedha za mikopo asilimia 10.
Aidha amepongeza, halmashauri kwa kutekeleza ilani kwa kutoa mikopo ya jumla ya fedha kiasi cha zaidi ya milioni 109 kwa vikundi 27 kati ya vikundi hivyo 18 ni wanawake , 6 ni vya vijana na vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu vimenufaika na mkopo huo.
Hata hivyo, amewataka watumishi wa umma kuwa mstari kuelezea miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt John Magufuli.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai