Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Said Irando ameagiza kuundwa kwa timu ya uchunguzi ikiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Hai SSP Juma Majatta kuchunguza madai ya kunyanyaswa kingono kwa watumishi wanaofanya kazi katika kampuni ya uzalishaji maua ya Deker.
Irando ametoa kauli hiyo hii leo wakati akisikiliza kero za wafanyakazi wanaofanya kazi katika shamba la maua la Deker ambapo wafanyakazi hao wamedai kunyanyaswa kingono na baadhi ya viongozi hao wanaowasimamia.
Akisikiliza kero hizo mkuu wa wilaya ya Hai Juma Irando amekemea vikali vitendo hivyo huku akisema kuwa ni kinyume na taratibu za kazi katika maeneo yote hapa nchini na kuwataka waajiri pamoja na viongozi kuwa waadilifu ili kuleta tija katika utendaji wa kazi.
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Hai Bi Upendo Wella amesema kuwa katika kurahisisha upatikanaji wa taarifa hasa zinazohusiana na vitendo vya unyanyasaji ni vyema uongozi ukaweka visanduku maalumu kwaajili ya kupokea maoni ya wafanyakazi hao badala ya kusubiri viongozi wa ngazi za juu kuja kubaini matukio kama haya.
Amesema kuwa uwepo wa masanduku ya maoni utasaidia kuwabaini kwa haraka wahusika wa vitendo hivyo pamoja na kutoa uhuru na usiri kwa mtoa taarifa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai