Katibu Tawala wilaya ya Hai Sospeter Magonera ametoa pongezi ameeleza kuridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kawaya Kati vinavyojengwa kupitia mradi wa BOOST.
Aidha Katibu Tawala Magonera ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za utekelezaji wa miradi na kuwataka wananchi kuilinda miradi hiyo itakapokamilika.
Magonera aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Hai kwenye ukaguzi wa miradi hiyo inayotekelezwa kupitia mradi huo ambapo shule hiyo imetengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 106, 300,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu matatu ya vyoo.
"Madarasa ni mazuri yanavutia, mimi toka nimefika kwenye wilaya hii ndiyo nimeona madarasa mazuri hapa Kawaya, majengo yapo mengi sehemu nyingi lakini hapa Kawaya mmetia fora, hivi ndivyo Serikali inataka, fedha zinazokuja ni nyingi kwa hiyo miradi lazima itekelezwe kwa ubora, angalau hapa wananchi wataona thamani ya fedha kwa sababu hizi ni fedha za wananchi na ubora huu ndiyo tunaoutaka" amesema DAS Magonera
Amewataka wananchi kuendelea kuchangia nguvukazi katika miradi hiyo ambayo ikikamilika italeta manufaa makubwa kwao"muendelee kuchangia nguvu zenu lakini vilevile muhakikishe kwamba ulinzi kwenye eneo hili la shule unakuwa mzuri na watoto wetu wanakuwa salama wakati wote"
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga amewataka mafundi kuendelea kutekeleza ujenzi huo kwa kuzingatia ubora na viwango pamoja na kukamilisha miradi kwa wakati nakusisitiza kuwa mafundi wanatakiwa kutoka katika eneo husika la mradi lengo likiwa ni kuwainua wananchi hao kiuchumi.
Kwa upande wake Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Hai Josiah Gunda amewataka wananchi kutembelea mara kwa mara miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili kujionea iwapo inatekeleza kwa ubora kwa lengo la kuisaidia Serikali kubaini mapungufu kwenye miradi hiyo ambayo ambayo huwanufaisha moja kwa moja wananchi hao.
Shule ya msingi Kawaya Kati imepokea fedha za mradi wa BOOST shilingi 106,300,000 ambapo 100,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa huku 6,300,000 zikielekezwa katika ujenzi wa matundu matatu (3) ya vyoo ambapo mradi ujenzi umefikia hatua ya plasta na fedha zilizotumika hadi hadi kufikia hatua hiyo ni 40,000,000 na kiasi kilichobaki ni 66,300,000 ambapo ujenzi unaendelea.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai