Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Saidi Irando amewataka wanafunzi kutokuwa na hofu badala yakwe wawe watulivu wakati wa kufanya mtihani ya kidato cha nne inayoonza leo.
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na kipindi cha siku mpya kupitia Boma Hai FM na kuwataka wanafunzi hao kufanya mtihani yao kwa umakini ili kuiweka wilaya ya Hai katika nafasi nzuri ya ufaulu kitaifa.
Irando amewaongeza kuwa kamati ya ulinzi na usalama imejipanga vema kuhkikisha kuwa mtihani huo unafanyika kwa usalama unaotakiwa na kwakufata taratibu zote na kuwataka wazazi kuendelea kuwapa sapoti na kuwatia moyo wanafunzi hao ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao
Naye Mbunge wa jimbo la Hai Ndg. Saashisha Mafue amwawashukuru wazazi na walezi wa watoto kwa kutii wito kwa kuwapeleka watoto shule ili waweze kutimiza malengo yao
Amewapongeza wanafunzi kwa hatua hiyo waliyofikia kwakua safari ya masomo yao yawezekana haikuwa rahisi kwakua wamejiepusha na vishawishi vingi wa kundi rika na kuwataka wakafanye vizuri kwa yale yote waliofundishwa.
Aidha amewashukuru viongozi mbali mbali kwa ushirikiano wao pamoja na kumshukuru Raisi wa jamhuri ya Muungani wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa fedha za ujenzi wa madarasa katika wilaya ya Hai.
Naye Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Hai mwl. Juliasi Wiliam Mduma amesema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kufanya mtihani huo yamekamilika na kuwataka wazazi kuwadhibithi watoto wanapo rudi nyumbai ili kujisomea na kutengeneza ufauli mzuri kwani ndo lengo la kila mzazi
Halmashauri ya wilaya ya Hai inategemea watahiniwa zaidi ya elfu tatu watafanya mtihani wa kidato cha nne ambapo wavulana ni 1353 na wasichana ni 1680 huku wanafunzi wanaojitegemea (private candidate) ni 155 ambapo wavulana ni 64 na wasichana ni 91 pia watahiniwa wa mtihani wa maarifa (q.t) ni 18 ambapo wavulana ni 10 na wasichana ni 8
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai