Afisa Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai Julias Kakyama amewataka wanafunzi wa Kidato cha Sita kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi ya muhimu ya Mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari uliopangwa kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni.
Akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule zenye Kidato cha Sita alipotembelea shule hizo kukagua wanafunzi wanaorejea kutoka nyumbani na kugawa vifaa vya kunawia kwenye shule hizo Kakyama amesema wanafunzi wanatakiwa kuutumia vizuri muda huu mfupi.
Amewasisitiza walimu na wanafunzi kushirikiana katika maandalizi ya mitihani ili wanafunzi waweze kufanya vizuri kwenye mtihani huku akisisitiza kuwa wanafunzi wajiwekee malengo ya kupata alamu za juu kujihakikishia ufaulu mzuri.
Kakyama amewaelekeza Wakuu wa Shule hizo kusimamia nidhamu ya wanafunzi na kuhakikisha kuwa juhudi za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona zinazingatiwa na wote.
“Serikali inathamini watu wake, mkiwemo ninyi wanafunzi na imepokea msaada kutoka kwa wahisani na kuamua kuwagawia bila kujali shule ya Serikali au ya binafsi au ya taasisi kwa sababu wote ni watanzania”
“Juhudu hizi za Serikali inabidi zikutane na juhudi za kila mmoja wenu za kujikinga binafsi na kuwakinga wengine ili vita ya ugonjwa huu ipiganwe kwa pamoja” Amesema Kakyama.
Aidha Afisa Elimu amezuia rihusa za kwenda nje ya shule kwa wanafunzi wote katika kipindi watakapokuwa shuleni na kwamba iwapo watakuwa na mahitaji ya muhimu washirikiane na wakuu wa shule ambao wataweka utaratibu wa kuwaletea huduma na mahitaji hayo.
“Ruhusa zote zimefungwa ikiwemo kwenda sehemu za ibada. Mkuu wa Shule atawawekea utaratibu wa kufanya ibada hapa shuleni. Mtasaidiwa namna ya kupata viongozi wa dini watakaoendesha ibada hapahapa shuleni kulingana na Imani na madhehebu yenu” Amesisitiza.
Afisa Elimu ametembelea shule 10 zenye wanafuzni wa Kitado cha Sita na kuzungumza kwa pamoja na walimu na wanafunzi huku akiwakabidhi vifaa vya kunawia mikono ikiwemo ndoo na sabuni 42 ili kuimarisha juhudi za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai