KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma ameipongeza Mamlaka ya Maji mijini na vijijini RUWASA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha wanawapatia maji safi wananchi hivyo kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Geraruma aliyasema hayo Juni 11 2022 wakati alipotembelea mradi wa uendelezaji wa Miundombinu ya Maji Safi wa mto Kikavu Wilayani Hai wenye thamani ya Shilingi bil 3.3
Alisema wametembelea mradi huo na kuona namna mamlaka hiyo ilivyofanya kazi nzuri kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo muhimu kwa ustawi wa maisha yao ya kila siku katika Mji wa Hai ambao umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya maji kutokana na ukuaji wa mji huo.
Kiongozi huyo aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha wanafikisha maji kwa haraka kwa wananchi ikiwemo kutekeleza majukumu yao kwa wakati pamoja na wananchi wanapolipia waweze kuunganishiwa kwa muda muafaka ili kuepusha malalamiko yasiyokuwa na tija.
Hata hivyo mkimbiza mwenge wa Uhuru aliwakumbusha wananchi kuhakikisha wanajiandaa kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kwani ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.
Mwenge wa Uhuru wilaya ya Hai,ulizindua ,kuweka Jiwe la msingi, kufungua na kakagua miradi kwa ajili ya kusogeza na kuboresha huduma kwenye jamii yenye thamani ya zaidi Shilingi bilioni 4.17
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai