• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Hai District Council
Hai District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hai

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Accounts and Finance
      • Utawala na Utumishi
      • Ardhi na Maliasili
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Usafi na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
        • Taarifa Idara ya Kilimo
      • Mifugo na Uvuvi
        • Wasilisho Mifugo
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Maporomoko ya Maji ya Nshara
      • Chemchemi ya Chemka
      • Mila na Utamaduni
      • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Industry and Trade
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Kilimo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Mipya
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu
      • Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi
      • Ahadi ya Uadilifu Watumishi
      • Fomu ya Maombi ya Likizo
      • OPRAS Walimu
      • OPRAS Watumishi
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Taarifa kwa Umma-Mikopo
    • Jarida
  • Mifumo
    • Mfumo wa Kiuhasibu (FFARS)
    • Mfumo wa Bajeti (Planrep)
    • Mfumo wa Vibali Safari za Nje
    • Mfumo wa Taarifa za Mapato (LGRCD)
    • Mfumo wa Taarifa za Shule (TanzaniaSIS)
    • Usajili Kupata TIN (TRA)

Korosho kuimarisha Uchumi Wilaya ya Hai

Imetumwa: May 17th, 2018

Wananchi wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kushiriki kwenye kilimo cha mazao ya biashara likiwemo zao la korosho ambalo limetambulishwa kwa mara ya kwanza wilayani hapo kwa uzinduzi uliofanyika tarehe 17/05/2018 kwenye jengo la Kituo cha Rasilimali za Kilimo (WARC) lililopo kata ya Masama Rundugai.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa zao hilo; Katibu Tawala Wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua miche inayogawiwa bure na serikali lakini pia kutoa maeneo yao kwa ajili ya kuotesha miche ya korosho kwani zao hilo ni moja ya mazao ya biashara yanayofanya vizuri kibiashara na litasaidia sana katika kuinua uchumi wa wananchi hasa wa ukanda wa tambarare.

“Natoa wito wa serikali kwa wananchi wa maeneo yatakayolimwa zao hili wakiongozwa na wenyeviti wa vijiji na viongozi wengine katika maeneo yao wahamasishane kuendelea kutenga maeneo ya kuotesha miche ya korosho ili kufikia lengo la kuotesha miche 5000 kwenye kila kijiji ili kuweza kuona tija na faida za zao hili” Amesema Wella.

Wella amewata wale watakaopatiwa miche inayogawiwa na serikali kuitunza vizuri kwenye mashamba watakapoipanda kwani serikali imetumia fedha katika kuandaa miche hiyo ili iweze kumfikia mwananchi bila gharama huku akiwaagiza wataalamu wa kilimo kuwafikia wananchi kwa ajili ya kuwapatia elimu na usaidizi wa kitaalamu wakati wa kutunza miti ya korosho kwa ajili ya kupata mavuno makubwa zaidi.

Akitoa salamu za wilaya kwa mgeni rasmi; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo amewapongeza wananchi wa kata ya Masama Rundugai kwa namna wanavyolitunza na kulitumia jengo la Rasilimali za Kilimo kwa ajili ya kupata elimu ya mambo yanayohusu kilimo.

Aidha Sintoo amewahimiza wananchi kuona umuhimu wa kulima zao la korosho ambalo halina gharama kubwa katika matunzo lakini pia ni zao la muhimu katika uchumi wa viwanda litakalobadilisha hali ya kiuchumi ya wananchi watakaolima zao hilo.

“Leo tunazindua rasmi kilimo cha korosho kwenye ukanda wa tambarare wa wilaya yetu; tuna furaha sana tumepata miche elfu 16 kutoka Bodi ya Korosho na tumeona vema kwanza tufanye shamba darasa kwenye eneo la heka 2 za Shule ya Msingi Rundugai litakalotumiwa na wataalamu wa kilimo kuwafundishia wakulima” ameongeza Sintoo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Masama Rundugai, Elibariki Mbise amewataka wananchi kupokea vizuri zao la korosho kwenye maeneo ya ukanda wa tambarare kwani ni sehemu ya kutunza mazingira lakini pia mavuno yatokanayo na zao hilo yatasaidia kuboresha uchumi wa wakulima huku akihusisha kwa karibu zao hilo na maendeleo ya viwanda.

“Zao hili lina manufaa makubwa mbali na kuwa ni zao kwa ajili ya biashara lakini pia ni sehemu ya kuhifadhi na kutunza mazingira kama mti lakini pia tumeona umuhimu wa zao hili kwa uchumi kwani bei ya kahawa na bei ya korosho zinakaribiana. Sasa ukanda wa juu kahawa na ukanda wa tambarare ni korosho” Amesisitiza Diwani Mbise.

Naye Afisa Kilimo wilaya ya Hai, David Lekei amebainisha sababu ya zao la korosho kulimwa ukanda wa tambarare kuwa ni kwa sababu ukanda wa tambarare unapata mvua kidogo na kukaa muda mrefu katika hali ya ukame kitu ambacho zao la korosho linahimili.

Lekei ameongeza kuwa hadi sasa yamepatikana maeneo ya kuotesha miche ya korosho kwenye vijiji 23 vya kata tisa kukiwa na jumla ya hekari 643 zilizo tayari kwa ajili ya kuotesha miche huku wakulima 450 wameshajitokeza kutaka kuotesha miche ya zao hilo.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Rundugai walioshiriki kwenye uzinduzi huo wamesema wanafurahi kuona zao hilo limefika kwenye maeneo yao na wanategemea watafaidika na mavuno ya zao hilo katika kuboresha hali yao ya kiuchumi.

“Kwa jinsi tunavyosikia wenzetu wa Mtwara na Lindi wanavyopata mazao mengi inatupa moyo na sisi kuwa tutapata mazao kwa ajili ya biashara ila tunaomba serikali iendelee kutuelimisha kuhudumia zao hili kitaalamu” amesema Mwanaisha Msuya mkazi wa Rudugai.

Uzinduzi wa kilimo cha korosho katika ukanda wa tambarare wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umefanikiwa baada ya kukamilika kwa utafiti uliofanywa na wataalamu na kuthibitisha kuwa maeneo hayo yanafaa kwa kilimo cha zao hili huku ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya serikali ya kufufua mazao makuu matano ya kibiashara ya Pamba, Chai, Tumbaku, Kahawa na Korosho hivyo kufanya Wilaya ya Hai kupata mzao makuu mawili ya Kahawa kwenye ukanda wa juu na korosho kwenye ukanda wa tambarare.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA YA UDEREVA March 28, 2025
  • TANGAZO LA MKOPO KWA WATUMISHI December 20, 2024
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA JIMBO LA HAI 2024 December 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA October 29, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • Shule Ya Msingi Nguzo Nne Yashika Nafasi Ya Pili Kwa Usafi

    April 09, 2025
  • Wananchi Wa Hai Wapo Tayari Kwa Uchuguzi

    April 05, 2025
  • Wananchi Wa Hai Wapo Tayari Kwa Uchuguzi

    April 05, 2025
  • Mkuu Wa Wilaya Ya Hai Ameongeza Anna Boniface

    March 24, 2025
  • Ona Yote

Video

UGAWAJI WA PIKIPIKI WILAYA YA HAI
Vidio Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Planrep
  • TANEPS
  • Mfumo wa Ajira za Afya
  • Blog ya Wilaya
  • Fomu ya Maombi ya Likizo
  • Fomu ya OPRAS - Walimu
  • Fomu ya OPRAS - Watumishi
  • Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba Shule za Wilaya ya Hai Mwaka 2020
  • Muundo wa Halmashauri

Viunganishi Vinavyohusiana

  • BARUA PEPE YA MALALAMIKO
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya serikali
  • TAMISEMI
  • Mfumo wa Bajeti

Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani

Wasiliana Nasi

    Kitongoji cha Bomani

    Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai

    Simu: 0754553560

    Simu ya Mkononi: 0754553560

    Barua Pepe: ded@haidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai