Wilaya ya Hai imezindua chanjo ya mifugo katika kata ya BOndeni ambapo kuku zaidi ya mia tatu zimepata chanjo hiyo .
Akizungumza wakati wa kuzindua chanjo hiyo kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Hai David Lekei amesema kuwa lengo la utoaji wa chanjo hizo za ruzuku kutoka serikalini ,ni kuwasaidia wafugaji kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya mifugo ikiwemo kideri na ndui
Ameongeza kuwa chanjo hizo zitawezesha wafugaji kufuga Kwa umahiri na kukuza sekta ya ufugaji ndani na nje ya nchi,na kuongeza Pato la Taifa na mtu mmoja mmoja .
Naye mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kingereka A Dastarn Kimaro
Amesema kuwa chanjo hizo zitawasaidia wafugaji kuondokana na hasara zinazotokana na ufugaji ambazo awali zilikuwa changamoto hasa magonjwa ya mifugo kama vile kuku na ng'ombe.
Mwenyekiti curt.....
Nae mwananchi ambaye ni mnufaika wa chanjo hiyo amesema kuwa chanjo hiyo imesaidia kupunguza gharama za ufugaji na kuwawezesha kufuga Kwa umahiri.
Mnufaika......
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai