Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai,
Ndg. Dionis Myinga, amekabidhi vishikwambi
kwa Maafisa Mifugo wa wilaya hiyo ikiwa ni
sehemu ya juhudi za kuboreshautoaji wa hudumakatika sekta ya mifugo.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Ndg. Myinga amesema kuwa hatua hiyo
inalenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa takwimu, ufuatiliaji wa afya za mifugo na
kuimarisha mawasiliano kati ya maafisa na
wafugaji.
“Vishkwambi hivi vitawawezesha maafisa wetu kukusanya taarifa sahihi za mifugo, kufuatilia
magonjwa kwa wakati na kuwasilisha taarifa kwa haraka kwenye makao makuu ya wilaya.
Ni hatua muhimu ya kisasa katika usimamizi wa mifugo hapa Hai,” amesema Dionis Myinga
Nae Mkuu wa divisheni ya kilimo, ufugaji na uvuvi, Ndg David Lekei amesema
“kuna zoezi la kitaifa la kudhibiti magonjwa
lililoanza mwezi wa saba hivyo vishkwambi hivi vitatusaidia sana katika kukusanya takwimu" hivyonaamini
Kwa upande wao, Maafisa Mifugo waliopokea
vishkwambi hivyo walishukuru na kuelezakuwa
vifaa hivyo vitarahisisha kazi zao za kila siku
mashinani na kupunguza urasimu wakaratasi.
Waliahidi kutumia vishkwambi hivyo kwa ufanisi ili kuwanufaisha wafugaji wa wilayaya Hai.
Hafla hiyo ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuendeleza matumizi ya teknolojia yakidijitali
katika sekta ya kilimo na mifugo kwa lengo la
kuongeza tija na kuhakikisha usalamawa chakula.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai