Kaimu mkurugenzi mtendaji wilaya ya Hai Rajabu Yateri amewapongeza maafisa ugani wa wilaya hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwaelimisha wakulima hasa wa maeneo ya vijijini ili kulima kilimo chenye tija.
Yateri ameyasema hayo katika mafunzo ya maafisa ugani yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo kwa lengo la kuwaongezea weledi juu ya mfumo wa M-Kilimo unaomwezesha mkulima kupata taarifa kwa wakati ili kutatua kero zinazohusu kilimo.
“Natambua umuhimu wa maafisa ugani, kwasababu hakuna namna mtanzania anaweza akakwepana na afisa ugani sijui kama yupo, kwasababu ninyi mnadili moja kwa moja na wakulima, kwahiyo kama asilimia 65 ya watanzania ni wakulima kwahiyo mnadili na watu ambao idadi yao ni kubwa sana”
Akizungumzia kuhusu mfumo wa M-Kilimo, afisa kilimo wilaya ya Hai Bw. David Lekei amesema “huu mfumo unafaida kubwa sana kwa sababu sasaivi Tanzania tunachangamoto ya maafisa ugani yaani watumishi wanaotoa elimu ya ugani kwa wakulima ni wachache ukilinganisha na wanaohitajika kwani wakulima ni wengi lakini watumishi ni wachache”
“Kwahiyo watumishi hawa wachache wanapoweza kuwasiliana na wakulima kupitia mfumo huu kwa njia ya mtandao wanaweza kuwafikia wakulima wengi tu wakiwa wamekaa tu labda nyumbani ama ofisini mkulima anauliza swali anajibiwa moja kwa moja kwahiyo inakuwa ni mawasiliano mazuri ya kutatua kero za wakulima wengi kwa wakati mmoja”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai