Serikali wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro imewataka maafisa ugani kutumia vema pikipiki walizopewa kwa ajili ya kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa wakati na kuwapatia huduma muhimu za ugani ili kuwawezeha kufanya kilimo chenye tija.
Kauli hiyo imetolewa Juni 14 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Hai ndugu Juma Irando wakati akikabidhi jumla ya pilipiki 39 kwa maafisa ugani wa halmashauri hiyo na kuwasisitiza kuzitunza pikipiki hizo ili ziweze kutumika kwa muda mrefu huku akiwakumbusha kuwa pikipiki hizo sio kwa ajili ya shughuli za kusafirishia abiria (bodaboda) na badala yake zifanye kazi iliyokusudiwa na serikali.
Kwa upande wake afisa kilimo wa halmahauri ya wilaya ya Hai ndugu David Lekei amesema kuanzia mwaka wa fedha Julai 2022 maafisa ugani hao watakuwa wakipatiwa fedha ya mafuta pamoja na matengenezo.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ndugu Edmund Rutaraka amewataka maafisa ugani hao kuwasimamia wakulima ili wafanye kilimo cha kibiashara baada ya changamoto hiyo ya usafiri kutatuliwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Hai ndugu Wang’uba Maganda amesema asilimia kubwa ya wananchi wa Hai ni wakulima na hivyo serikali imeamua kuwawezesha maafisa ugani ili kufika katika maeneo yao ya kazi kwa urahisi.
Utoaji wa pikipiki hizo ni mpango wa serikali kupitia wizara ya kilimo ulio lenga kuwawezesha maafisa ugani wote nchini kupata urahisi wa kuwafikia wakulima na Halmashauri ya wilaya ya Hai ni miongoni mwa halmashauri zilizonufaika na mpango huo ambapo jumla ya maafisa ugani 39 wote wamepata pikipiki.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai