Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Juma Irando amewataka maafisa watendaji wa kata na vijiji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mikataba ya lishe katika ngazi ya kata na vijiji wilayani humo lengo likiwa ni kukabiliana na lishe duni na kupunguza athari za utapiamlo kwenye jamii.
Irando ametoa kauli hiyo Juni 29 aliposhiriki kusaini mikataba ya lishe iliyosainiwa baina yake na watendaji wa kata na vijiji kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na shilingi 1000 itakayotolewa kwa kila mtoto kwajili ya lishe.
Kwa upande wake kaimu Afisa lishe wilaya ya Hai Hepiphania Laiza akieleza tathmini ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya kata na vijiji katika wilaya ya Hai kuanzia Julai 2021-Juni 2022 ameeleza kuwa wao wana wajibu wa kuhakikisha kuwa lishe ni ajenda ya kudumu katika vikao vya kamati za maendeleo.
Aidha utekelezaji wa shughuli za lishe hutegemea fedha zinazotengwa katika bajeti ya halmashauri ya mwaka ambapo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022 wilaya ya Hai ilitenga zaidi ya shilingi million 49 kwa ajili ya watoto 35,194 wenye umri chini ya miaka mitano.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai