Serikali imetoa jumla ya shilingi 70,100,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 ya awali ya mfano katika shule ya msinngi Nkwanara kijiji cha Kyeeri kata ya Machame Magharibi kupitia mradi wa BOOST.
Akizungumza wakati akitambulisha mradi huo kwa wananchi,mratibu wa Boost wilaya ya Hai ndugu Japhari Zaidi amesema pamoja na madarasa hayo pia kitajengwa choo chenye matundu sita na sehemu ya watoto kuchezea.
Zaidi amezitaka kamati Pamoja na viongozi kuhakikisha fedha zilizotolewa na Serikali kutekeleza mradi huo zinatosheleza na kutoisababishia serikali madeni yasiyo kuwa ya lazima.
“tumepokea shililini milioni 70 na 100,000 niombe fedha hiyo iende ikatekeleze mradi mwanzo mwisho na kukamilisha mradi ,hakutakuwa na fedha yoyote ya ziada kutoka mahala popote endapo mradi utakuwa haujakamilika”
“Isisje ikafika wakati mnamsumbua mhe Diwani, Mwenyekiti pamoja na Mtendaji kwenda kubambua wananchi kwa ajili ya kuchangia fedha za kukamilisha mradi”alisisitiza Zaidi.
Ndugu Zaidi amewataka wajumbe watakao teuliwa katika kamati mbali mbali za utekelezaji wa mradu huo pamoja na Serikliali ya kijiji na wananchi kuhakikisha kuwa vifaa vinatunzwa na vinatumika kama ilivyo kusudiwa.
Akizungumza kwa naiba ya wenzake ndugu Tegemea Swai ameishikuru serikali kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi na kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano kipindi chote cha utekelezaji wa mradi huo.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Martin Munisi ameishukuru serikali kwa kutoa kiasi hicho cha fedha ambacho kitabadilisha tawira nzima ya shule hiyo.
“tunamshukuru sana Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha hizi ,tunamshukuru Mbunge wa Jimo la Hai Saashisha Mafue kwa ufatiliaji wake na nipende kuwajulisha tu wananchi kuwa mbali na fedha hizo pia halmashauri imetutengea shilingi milioni 16 kwa ajili ya ujenzi wa choo katika shule hii hivyo tatizo la vyoo litakwisha kabisa”
Munisi pia amemtaka Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kutokubali kuyumbishwa na yeyote wakati wa utekelezaji wa mrdi huo bali asimamie sheria,taratibu,kanuni na miongozo ya serikali.
Hivi karibuni halmashauri ya wilaya ya Hai imepokea kasi cha shilingi 773,100,000 kwa ajili ya uboreshaji wa mazingira ya kujifunzi kupitia mradi wa BOOST ambapo shule ya Nkwanara ni miongoni mwa shule zilizo nufaika.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai