Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 ya mfano ya awali katika shule ya msingi Mafeto kupitia mradi wa Boost iliyo katika Kijiji cha Mbosho kata ya Masama Kati wilayani Hai.
Akizungumza wakati wa kutambulisha ujenzi wa madarasa hayo,Mratibu wa Boost wilaya ya Hai Jafari Zaid amesema fedha hizo zitatumika kujenga madarasa mawili, matundu sita ya vyoo na sehemu ya Watoto kuchezea.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi na na Awali wilaya ya Hai Huseein Kitingi amewataka viongozi wa Kijiji hicho kuhamasisha wananchi kujitolea nguvu kazi katika ujenzi wa madarasa hayo,ikiwa ni Pamoja na kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya ujenzi vinakuwa salama nyakati zote za ujenzi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Masama Kati, mhe. Kandata Kimaro amemshukuru mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za mradi katika kata hiyo ,miradi ambayo inatatua changamoto mbali mbali za wananchi.
“napenda Kumshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi za miradi ,huu ni mradi wa nne katika kata hii,mingine tayari 3 tayari imeanza,namshukura pia Mhe Munge wa Jimbo la Hai kwa kufuatilia sana fedha za mradi katika wiliaya yetu”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai