Baraza la halmashauri ya wilaya ya Hai limemshukuru Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi cha shilingi Bil 1.5 z kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara za vijiji na mitaa katika wilaya ya Hai, lengo likiwa ni kurahisisha usafiri kwa wananchi wakiwemo wakulima walioko maeneo ya vijijini.
Baraza hilo limetoa shukrani hizo baada ya taarifa iliyotolewa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo Novemba 2, 2021 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai na Meneja wa TARURA wilayani HAI ndugu Rickson Lema juu ya serikali kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Edmund Rutaraka baada ya kupokea taarifa hiyo amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imetenga fedha hizo ili kutengeneza barabara hizo kwa kiwango cha changarawe ili ziweze kupitika kwa urahisi kuwafikia wakulima na hivyo tunamtaka menejeza wa TARURA wilayani humu kuishirikisha halmashauri katika utekelezaji wake kama ambavyo ameelekezwa.
“Tulikuwa tunajadili ni jinsi gani tunaweza kutumia Bilioni 1.5 zilizotolwa na Mama Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vijiji na mitaa zile ambazo zinashida kwelikweli kwa kuwa maelekezo ya Mhe. Tunatengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe ili barabara ziweze kupitika vijijini kuwafikia wakulima kuchukua mazao yao na kuyapeleka sokoni” alisema Rutaraka.
Aidha Rutaraka akizungumzia kuhusu mapato ya Halmashauri hiyo amesema kuwa hadi kufikia mwezi septemba halmashauri hiyo ilifikia asilimia 21 na kuwataka madiwani kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuendelea kuboresha katika eneo hilo.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Muyinga amewataka madiwani na watumishi kushirikiana katika kufanya jitihada za kusimamia ukusanyaji wa mapato sambamba na kudhibiti upotevu wa mapato ya halmashauri hiyo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai