Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Hai limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu kwa kuwapatia mashine ya X-ray katika kituo cha Afya Longoi yenye thamani ya shilingi milioni 160.
Kituo cha Afya Longoi ni moja ya vituo vipya katika wilaya ya Hai ambacho kimejengwa kwa fedha jumla ya shilingi milioni 600 kutoka Serikalini ambapo awali halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kujenga majengo ya mwanzo na baadaye milioni 200 kwa ajili umaliziaji.
Akizungumza kaika kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri Edmund Rutaraka amesema kuwa mashine hiyo ya X-ray inakwenda kuhudumia kata 4 za wilaya hiyo ikiwemo kata ya Weruweru, Rundugai, Mnadani pamoja na kata ya Masama Kusini kwa upande wa kwa Sadala ikiwa ni kilomita chache kwenda Longoi.
Kwa upande wake mkuu wa divisheni ya huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na lishe Dkt. Etikija Msuya ameeleza kuwa mashine hiyo ni muhimu katika hospitali hiyo kwani itasaidia katika kuyatambua magonjwa mbalimbali hasa yale yanayohusiana na mfumo wa upumuaji.
“tunaishukuru sana Serikali kwa kutupatia mashine hii kwasababu itasaidia wananchi wote wanaoishi ukanda huu wa bondeni kwani huduma hii imesogea karibu na wananchi wa Masama Rundugai ambapo itanufaisha hadi kata za jirani”
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai