Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wameishukuru serikali kwa kutoa fedha za miradi kwa ajili ya kujenga na kukamilisha ujenzi wa madarasa na zahanati katika maeneo yao.
Wakizungumza leo katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa za kata , madiwani hao wamesema ukamilishaji wa madarasa hayo umesaidia kupunguza upungufu wa madarasa katika maeneo yao na kuomba serikali kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa madarasa hasa kwa shule za muda mrefu.
Akizungumza katika kikao hicho diwani wa kata ya Machame Uroki Roy Swai amesema miongoni mwa miradi iliyotekelezwa katika kata hiyo ukamilishaji wa ujenzi wa darasa katika shule ya Nkwasaringe, maabara shule sekondari Neema hali ambayo imeboresha mazingira ya kujifunzia.
Kwa upande wake ndugu Nasibu Mndeme diwani wa kata ya Mnadani ameishukuru serikali kwa kutoa fedha za kukamilisha nyumba ya mtumishi yenye uwezo wa kuchukua familia mbili kwa wakati mmoja katika Kijiji Kwatito na ujenzi wa choo, ujenzi wa maabara na vyumba viwili vya maabara katika Kijiji cha Shiri njoro pamoja na miradi mingine inayoendelea katika kata hiyo hali ambayo imepunguza mzigo wa michango ya fedha kutoka kwa wananchi.
Akizumza wakati wa kufunga kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri hiyo ndugu Edmund Rutaraka amewataka madiwani kuwashirikisha pia wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wanaotoka kwenye maeneo yao kuweza kuchangia maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa na vyoo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai