Madiwani Kushiriki Kutokomeza Rumbesa Wilaya ya Hai
Imetumwa: February 24th, 2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameomba madiwani kushiriki kukemea wafanyabiashara wanaowanyanyasa wakulima kwa kununua mazao mashambani kwa vipimo visivyo sahihi vya rumbesa.
Akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani leo 23 Februari 2021, Sintoo amesema kufuatia malalmiko ya wakulima kuendelea kunyanyaswa na wafanya biashara atafanya ziara ya kutembelea masoko yote yaliyopo wilayani hapo ili kutatua changamoto hiyo.
“Nitapita katika masoko yote ya wilaya ya Hai kuangalia changamoto zao ikiwa ni pamoja na kukataza rumbesa zinazolalamikiwa na wauzaji, Madiwani nanyi mnawajibu wa kukemea rumbesa zinazonyanyasa wananchi wengi” Amesema Sintoo.
Amesema Kila Diwani kwenye kata yake akishiriki kikamilifu tatizo hilo la rumbesa litapungua na hatimaye kumalizika kabisa.
Kauli hiyo ya Mkurugenzi imekuja baada ya diwani wa kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani kutoa taarifa ya baadhi wa wafanyabiashara kuendelea kununua bidhaa za chakula kwa rumbesa jambo ambalo liwaathiri wakulima.