Kamati ya fedha imeridhishwa na ujenzi wa madarasa mawili yaliyojengwa katika shule ya msingi makeresho iliyopo katika kata ya Machame Magharibi,ukarabati na ukamilishaji wa chuo cha ufundi Chekimaji kilichopo katika kata ya Masama Rundugai pamoja na ujenzi unaoendea katika Hospitali ya wilaya ya Hai.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyofanywa na kamati hiyo, mwenyekiti wa halmashauri Edmund Rutaraka alisema kamati imefurahia na ujenzi wa miradi hiyo ambayo imetekelezwa kwa ubora na kwa kuhusisha kamati za ujenzi kwa kiwango
Kinachotakiwa. “Mimi nimefarijika kwa ujenzi wa mradi huu wa madarasa mawili makeresho kazi iliyofanyika ni kazi nzuri , utekelezaji wake ni mzuri ikilinganishwa na miradi mingine, pia nimpongeze diwani wa kata hii kwa usimamizi na ufuatiliaji kwa karibu wa mradi huu” alisema Rutaraka
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo James Mushi alimshukuru mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo yaliyokuwa chakavu.
“nimshukuru pia mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue kwa kuomba na kufuatilia
fedha hizi, aliomba tupate madarasa manne na sasa tumepata haya mawili. Niishukuru halmashauri ya wilaya ya Hai kwa kukubali mradi huu ukaletwa hapa ,niwashukuru pia viongozi wa chama cha Mapinduzi kata ya Machame Mashariki ambao tumeshirikiana bega kwa bega katika kufuatilia ujenzi wa madarasa haya”alisema Mushi.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo Nasibu Mndeme aliwataka viongozi kuwashirikisha wananchi katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuchangia nguvu kazi au fedha kadri watakavyokubalina kwenye vikao vyao hali ambayo itawafanya kujiona ni sehemu ya mradi.
Ujenzi wa madarasa mawili ya Makerosho yamegharimu kiasi cha shilingi 40,00
fedha ambazo zimetolewa na serikali kuu baada ya Mbunge wa jimbo la Hai kutoa maombi hayo katika ziara ya Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) huku ukarabati na ukamilishaji wa chuo cha ufundi cheki maji ukitekelezwa kwa kiasi cha shilingi 36,111,264 fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na ujenzi unaoendela katika hosptali unagharimu kiasi cha shilingi 1,044,056,630 kati ya hizo jengo la maabara linajengwa kwa kiasi cha shilingi 236,029,152,jengo la stoo ya dawa kiasi cha shilingi 192,733,205,upanuzi wa wodi ya wazazi 125,741,462,jengo la wodi daraja la kwanza 210,141,322 na walk ways shilingi 279,411,489.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai