MADIWANI wanne waliochaguliwa katika chaguzi mbili ndogo katika jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro wamekabidhiwa vyeti vyao vya ushindi na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Hai Yohana Sintoo.
Madiwani waliokabidhiwa vyeti ni wale waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Septemba 16 mwaka huu, ambapo mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Robsoni Kimaro kutoka kata ya Machame Uroki na ndugu Yohana Laiza (CCM) ambao wote walishinda kwenye maeneo yao.
Pia katika waliokabidhiwa vyeti ni madiwani wa kata ya Romu Shimiliafoo Kimaro na diwani wa kata ya Masama Kusini Elibariki Mbise ambao walipita bila kupingwa katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika Oktoba 13 mwaka huu.
Akiwakabidhi vyeti hivyo, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Hai Yohana Sintoo ameeleza kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu huku kila chama kikifuata taratibu zote zilizokuwa zikitarajiwa katika uchaguzi
“Uchaguzi ulifanyika kwa wazi na hakuna chama chochote kile ambacho kimeonyesha kutokuridhika na matokeo hali hii inaonesha ni jinsi gani demokrasia imekua katika jimbo hili” amesema sintoo.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Hai Kumotola Kumotola amewashukuru wananchi kwa kuendelea kukiamini chama cha CCM kwa kukipa ushindi hii ikiwa ni matunda ya matokea ya utekelezaji ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.
Kwa upande wao madiwani wateule wakizungumza kwa nyakati tofauti wameonesha kufarijika na namna wananchi wa kata zao walivyoonesha Imani na CCM na kuichagua kuwawakilisha kwenye vikao vya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai na kuahidi kuwatumikia wananchi kwa nguvu na akili zao zote katika kusimamia upatikanaji wa maendeleo katika maeneo yao.
Diwani Mteule wa kata ya Kia Yohana Laiza amebainisha kuwa yupo tayari kushirikiana na madiwani wenzake katika kufanikisha kazi kuu ya kupunguzia wananchi kero wanazokutana nazo kwenye maisha.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai