Maafisa elimu kata 17 pamoja na waalimu wa ushauri na unasihi kutoka shule zote za sekondari wilaya ya Hai wamepewa mafunzo ya Mpango wa Shule Salama Kwa kwa elimu ya sekondari yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mafunzo hayo yamefanyika leo kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundisha wanafunzi wa sekondari katika kuwezesha upatikanaji wa elimu bora na stadi za maisha ili waweze kukamilisha mzunguko wao wa elimu.
Msimamizi wa mafunzo hayo ambae pia ni afisa elimu kata, kata ya Rundugai Sebastian Mkambi amesema kuwa mafunzo hayo yanawajengea wanafunzi mazingira ya kujiamini, kujitambua, kujieleza na kujilinda dhidi ya ukatili wa aina mbali mbali.
Aidha amesema kutokana na kuwepo kwa matukio yaliyo kinyume na maadili watawafikia pia wanafunzi waliopo katika mabweni kwa ajili ya kuwapa ushauri na unasihi wa kiroho pamoja na kisaikolojia na sio kuwapa adhabu.
Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo Irene Mushi ambae ni mwalimu wa shule ya sekondari Hai amesema wao kama waalimu wamejifunza mambo mengi ambayo mwanzo awakuyafahamu kwa upande wa malezi ya watoto ikiwa ni pamoja na namna ya kuwashauri katika masomo yao ili wanufaike katika maisha yao ya baadae.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai