Katibu Tawala Wilaya ya Hai Sospeter Magonera ameipongeza Idara ya ardhi wilayani humo kwa kutoa hati miliki nyingi za kimila na za mijini kwa mwaka 2022/2023.
Ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani la kuwasilisha taarifa za kata, na kuongeza kuwa upatikanaji wa hatimiliki itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi ambayo inasasbabishwa na wananchi kutokuwa na nyaraka sahihi za kumiliki maeneo yao.
Magonera amewataka waheshimiwa madiwni na watendaji wa Kata kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na hati.
Amesisitiza kuwa upatikanaji wa hatimiliki hizo zitapunguza migogoro mingi ya ardhi na kuwawezesha wanachi kutumia muda wao katika kazi za uzalishaji.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai