Mahakama Wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro imewataka wananchi kuutumia mfumo mpya wa Usimamizi wa Wawatetezi (TAMS)Unaopatikana kwenye tovuti ya Mahakama Tanzania ili kuwabaini mawakili husika kama wanaruhusiwa kufanya Kazi ya Uwakili au hawaruhusiwi.
Hayo yamesemwa Leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai Mhe.Devoter Msofe ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za kilele cha wiki ya Sheria iliyofanyika Katika MAHAKAMA ya Mwanzo wilayani Hai.
Mhe.Msofe amesema kuwa Siku za hivi karibuni kumezuka wimbi la watu wanaojifanya kuwa ni mawakili na kufanya Kazi za uakili kinyume na utaratibu jambo linalopelekea kuwatapeli wananchi.
Amesema "Katika kuhakikisha kuwa tunadhibiti wimbi la watu wanaojifanya kuwa mawakili au wanaofanya Kazi ya uwakili kinyume na taratibu mahakama imeweka mfumo wa TAMS ambao ni mfumo wakumtambua Wakili husika, na mfumo huo upo kwenye tovuti ya Mahakama ambayo ni www.Judiciary.go.tz".amesema Mh.Msofe.
Kutokana jambo hilo mahakama imeweka mfumo huo wa Tanzania Advocates Management System (TAMS) Utakao wawezesha wananchi kuutumia ili kuwatambua mawakili husika kama wanaruhusiwa kufanya Kazi hiyo ama haruhusiwi huku akisistiza wananchi kuutumia ili kujiepusha na matapeli Hao.
Pia amesema kuwa katika kuimarisha uwazi na uadilifu Mahakama imekuwa ikitoa Elimu kwa Umma juu ya Athari za Rushwa na Kusisitiza katazo la kutoa Rushwa ili kununua Haki ndani ya Mahakama huku ikisistiza umuhumu wa maadili kwa watumishi wake.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai