Michuano ya mashindano ya Mbunge wa Jimbo la Hai , mkoani Kilimanjaro, Saashisha Mafuwe yamefikia tamati toka yalipoanza mwezi Agost 2022 kwa ya kata ya Mnadani ya Maili Sita fc kutwaa ubingwa huo.
Timu ya Mailisita itwaa ubingwa wa Mashindano ya Saashisha Cup 2023 baada ya kuibwaga timu ya Machame City kutoka kata ya Machame Kaskazini kwa jumala ya mabao 2-0 mcezo ulio chezwa katika uwanja wa chuo cha Ufundi Hai.
Mgeni rasmi katika fainali hizo , Naibu Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamisi Mwinjuma (MB) amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha sekta ya michezo nchini kwa kufanya maboresho ya miundombinu ya michezo hususani viwanja viliko vijijini .
Amesema mpango wa uboreshaji wa miundombinu ya michezo itasaidia kuibua vipaji kuanzia ngazi za mitaa kijiji , kata wilaya ,mkoa na hata taifa kwa maeneo mengi ya vijiji kumekuwepo na vijana wenye vipaji lakini wanashindwa kuvionyesha kutoka na kukoseka kwa viwanja vyenye sifa .
Naibu wa Waziri Mwinjuma amempongeza mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe kwa kuanzia mashindano hayo kwani yameleta mshikamo na umoja kwa wananchi bila kujali itikali za vyama vyao vya kisiasa .
“Nikupongeze sana mheshimiwa Saashisha kuwa kuanzia mashindano hayo bali na kujenga umoja na mshikamo kwa jamii pia yamesaidia kuibua vipaji vya soka kwa vijana wa jumbo lako na Tanzania kwa jumla yamesaidia kuepusha maswala ya kiuhalifu ”.
Mbunge wa jimbo la Hai, Mafuwe amesema mashindano hayo niendelevu na lengo ni kuipua vipaji vya vijana na kuviendeleza kwa kuwatafutia vilabu vikubwa hapa nchini kwa ajili ya majaribo na hatimaye kusajiliwa.
Akizungumza katika fainali hizo mkuu wa Wilaya ya Hai, Amiri Mkalipa amesema mashindano hayo yamesaidia vijana kuachana na mambo yasiyofaa katika jamii huku akisisitiza kwamba kazi ni msingi mkubwa wa maendeleo.
Awali akitoa taarifa ya mashindano hayo, Mwenyekiti wa chama cha Mpira wilaya hapa (HADFA) Omary Mlekwa amsema kuwa jumla timu 84 zilishiriki mashindano hayo yaliyoanzia ngazi ya kata
Mlekwa amesema bingwa wa mashindano hayo aliibuka na kitita cha shilingi laki tano ,jezi seti na mpira mmoja pamoja na kombe huku wachezaji wote wakivalishwa medali , Mshindi wa pili katika mashindano hayo timu ya Machame City alijitwalia kitita cha shilingi laki laki tatu , jezi seti moja , na mpira pamoja na medali kwa kila mchezaji.
Mshindi wa tatu katika mashindano hayo timu ya Lambo fc ilijipatia mpira mmoja na shilingi laki mbili, na timu ya nne Orori ilijipatia kiasi cha shingi laki moja na mpira mmoja.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai