Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Hai na kuzindua jengo la wodi ya wanawake katika hospitali ya wilaya ya Hai ikiwa ni utekelezaji wa kazi za Serikali unaofanywa na serikali ya wamu ya Tano chini ya Dr John Pombe Magufuli.
Akizindua wodi hiyo ambayo imejengwa kwa fedha zinazokusanywa na hospitali hiyo kupitia bima ya Afya makamu wa Rais amepongeza ujenzi huo na kusema ni jambo la mfano na la kuigwa huku pia akiwasihi wahudumu wa afya kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu ili kujipatia thawabu kwa Mungu.
Katika hatua nyingine makamu wa Raisi amehutubia mamia ya wananchi waliokusanyika katika eneo la ofisi ya kijiji cha Kwasadala huku akisifu jitihada zinazofanywa na halmashauri kupitia Mkuu wa Wilaya hiyo Lengay Ole Sabaya ambapo amesema kuwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato kimeongezeka kwa zaidi ya 200%.
Aidha pia makamu wa Rais amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wanaosababisha migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na vyama vya ushirika.
Makamu wa Rais amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro ambapo alitembelea wilaya mbali mbali kuanzia Alhamisi iliyopita ambapo pia makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; William Lukuvi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Suleiman Jaffo.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai