Katibu Tawala wa Wilaya ya Hai Upendo Wella amewataka washiriki wa mafunzoya makarani na wasimamizi wa maudhui wa sensa ya watu na makazi 2022 wilayaniHai, kuthamini na kutambua nafasi waliyopewa na serikali ya kusimamia zoezihilo.
Wella ametoa rai hiyo leo wakati wa ziara ya kamati ya ulinzi na Usalama yakutembelea mafunzo yanayoendelea katika vituo mbali mbali wilayani humona kusisitiza washiriki hao kutambua kuwa serikali imetumia fedha nyingikatika kutekeleza zoezi hili na hivyo kuwataka kuifanya kazi hiyo kwa umakiniili kuliwezesha taaifa kupata takwimu sahihi.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayaniHai ndugu Josiah Gunda amewataka washiriki kutunza vifaa vyote walivyokabidhiwakw ana kuzingatia maelekezo yote waliyopewa juu ya utunzaji wa vifaa hivyo.
Amesisitiza washiriki hao kuhakikisha kuwa wanafuata maadili ya Utumishi waUmma pamoja na sheria zake ikiwa ni pamoja na utunzaji wa siri za taarifa zotewanazopewa na wanakaya, mavazi nadhifu na matumizi ya lugha nzuri kwa jamii.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai