Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga ametoa rai kwa makarani wa Sensa wilayani humo kuzingatia nidhamu na maadili kwenye zoezi hilo litakalofanyika kuanzia Agosti 23 2022 nchini kote.
Myinga ametoa rai hiyo alipozungumza na Makarani hao walipokuwa wakipatiwa mafunzo kwa takribani siku 16 na kuwataka wawe wazalendo.
Kwa upande wake kamanda wa TAKUKURU wilayani humo Josia Gunda amewaambia Makarani hao wa Sensa waende wakaifanye kazi hiyo kwa uzalendo wa hali ya juu kwa zoezi hilo limegharimu Serikali fedha nyingi.
Aidha mwezeshaji wa mafunzo hayo Japhari Zaidi amewataka Makarani wa Sensa wanaotumia kilevi kuacha kutumia kwa kipindi hiki ili kuepuka kutia dosari zoezi hilo.
"Twende tukaitumikie nchi yetu kwa kufanya kazi hii kwa weledi na nidhamu, bia ni tamu lakini inaweza kugeuka chungu endapo utakunywa, utalewa na kupoteza nyaraka za Serikali" anasema Japhari
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Baraka Owenya amewaambia Makarani hao kuwa "Kitu cha thamani mnachoweza kutufanyia ni kwenda kufanya kwa uaminifu zoezi la Sensa lililopo mbele yetu, taifa limetuthamini limetumia fedha nyingi kuhakikisha zoezi hili linafanyika"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai