Mwenyekiti wa kamati ya Sensa wilaya ya Hai na Mkuu wa wilaya ya Hai Juma Irando amefunga rasmi mafunzo ya Sensa wilayani humo na kushuhudia viapo kwa Makarani wa Sensa,Wasimamizi wa mahudhui na Wasimamizi wa TEHAMA .
Akifunga mafunzo hay oleo Agosti 18, Irando amewataka Makarani kwenda kuwa mabalozi wazuri wa Sensa inayotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu na kuhesabu watu watakaolala ndani ya mipaka ya nchi bila kumwacha hata mmoja.
“tunaamini mtakwenda kufanya vizuri zoezi lililopo mbele yetu ,mkitoka hapa tunategemea mkawe mabalozi wazuri wa Sensa ,watu waliopo nje wanaamini zaidi maelezo kutoka kwako kwa kuwa umeapa”amesisitiza Irando.
Naye mjumbe wa Kamati ya Usalama wilaya ya Hai na Mjumbe wa kamati ya Sensa wilaya Mkuu wa Polisi hiyo SSP Juma Majatta ameelezea kuwa wanategemea zoezi hilo litafanywa kwa ufanisi wa hali ya juu likiwa ni kupata takwimu sahii kwa maendeleo ya nchi.
“kamati ya Sensa tunategemea ufanisi wa hali ya juu katika yale ambayo mmejifunza ili mwisho wa siku nchi yetu ipate Takwimu ambazo ni sahihi kwa ajili ya maenedeleo”
“Dakika chache zilizopita mmeapa na kiapo mlichohapa ni kwa mujibu wa sharia ,sasa si suala la kutishiana ni suala la kukumbushana ,utakapokwenda kinyume na kiapo jukumu letui sisi kama kamati ni kukuchota tu,tutakuchota” amesisitiza Majatta
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai