Wakuu wa wilaya nchini wametakiwa kutenga muda wao kwa kushirikiana na watendaji wengine wa serikali katika kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zilizopo katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa na katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Paul Makonda wakati aliposimama na kuzungumza na wananchi wa wilaya ya Hai katika eneo la kwasadala.
"Katika ziara yangu maeneo mbalimbali tumekutana na kero za wananchi katika maeneo mbalimbali, leo nitoe maelekezo kwa wakuu wote wa wilaya nchini na haya ni maelekezo ya chama; nendeni katika maeneo yenu mkawasikilize wananchi na kutatua kero zao".
Awali akizungumza mbele ya katibu mwenezi wa CCM taifa, Mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe ametoa salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha mbalimbali alizozitoa na anazoendelea kuzitoa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Hai.
Aidha pia Saashisha ametumia nafasi hiyo kumwomba katibu mwenezi Paul Makonda kumkumbusha Rais Samia kuhusu ahadi ya kujenga soko la kisasa kwa sadala ambapo ahadi hiyo ilitolewa wakati wa kampeni.
"Tumepata fedha nyingi katika miradi ya maji, elimu, afya, barabara lakini nikuombe umkumbushe Rais wetu mpendwa Dkt.Samia juu ya ahadi ya kujenga soko la kisasa hapa kwa sadala na tunaimani mama Samia atafanya jambo".
Ziara ya Paul Makonda katibu wa itikadi na uenezi wa CCM imehitimishwa leo mkoani Kilimanjaro ambapo ameelekea mkoani Arusha kuendelea na ziara.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai