Wananchi wa Kata ya Masama Rundugai wameishikuru serikali kwa ujenzi wa tanki la maji la lita 100,000 katika eneo la Kilimambogo kata ya Bondeni wilayani Hai.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa tanki hilo wakati wa mbizo za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023,wananchi hao wamesema kwa kujengwa kwa tanki hilo kutawaokolea gharama na muda walio kuwa wakitumia kutafuta maji kwa ajili ya matumzi way a familia zao.
Wamesema wakati mwingine wanafunzi walikuwa wakikosa masomo kwa sababu ya kutafuta maji umbali mrefu jambo ambalo lilikuwa linaadhiri mahudhuri ya watoto shuleni.
Kwa muijibu wa mkuu wa wilaya ya Hai miradi huo unalenga kutatua kero ya maji safai na salama kwa wananchi 9500 wa vijiji vya Kawaya ,Rundugai, Chekimaji, Kilimabogo na chemka
Akisoma taarifa wakati wa Mbizo za Mwenge wa Uhuru wilayani Hai, Meneja wa Wakala wa maji safi na Usafi wa Mazingira Emmanuel Mwampashi amesema serikali ilitoa kiasi cha shilingi 100,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa tanki hilo lililojengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 97.6.
Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge Abdalla Shaib Kaim, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo kujengwa kwa ubora unaotakiwa huku thamani ya fedha iliyotumika ikionekana.
“Kwa dhati kabisa baada ya kupongeza Serikali nichukue fursa hii kukupongeza wewe mhe Mkuu wa wilaya ukiwa msimamizi wa shuguli za miradi katika wilaya yako unafanya kazi kubwa kabisa na unatuheshimisha”,amesema Kaim.
‘tumefanya ukaguzi wa kina wa mradi na nyaraka kwa lengo la kujiridhisha endapo mradi umezingatia viwango vya ubora na kama thamani inaakisi na kuendana na mradi,itoshe kusema katika mradi huu tumejirisha na mradi umejengwa kwa kiwango bora kabisa”.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Hai, Sashisha Mafue amesema ujenzi wa mradi huo utakuwa kichocheo cha shuguli za kichumi kwa kuwaokolea muda wanachi wa vijiji hivyo muda.
Tanki hilo la maji lenye ujazo wa maji lita 100,000 linatarajiwa kuwanufaisha wanachi 9500
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai