Jeshi la polisi wilaya ya Hai wanatarajia kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za manaume yatakayo fanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 27 ya mwaka huu wa 20224 katika uwanja wa Uzunguni uliopo Bomang’ombe wilayani Hai.
Akizungumza leo hii tarehe 10/07/2024 na Redio Boma hai Fm mratibu msaidizi wa jeshi la polisi wilaya ya Hai Jeremia Mwandute amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kutoa mafuzo kwa jamii kuepukana na matukio mbali mbali ya kihalifu yanayondelea kutokea katika jamii zetu.
Amesema mashindano hayo yanayojulikana kama MASHINDANO YA POLISI JAMII hayana gharama yoyote kwa timu zinazoshiriki na zitashiriki timu nane kutoka katika wilaya ya Hai hivyo kuwataka mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano hayo.
Hata hivyo Mkaguzi msaidizi wa polisi wilaya ya Hai Fadhil Kayinga amesema kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atapewa kombe pamoja jezi seti moja, mshindi wa pili mipira miwili pamoja na zawadi binafsi kama mchezaji bora,mfungaji bora,kipa bora pamoja na mchezaji mwenye nidhamu.
Aidha Martine Katwiga ambae pia ni msaidizi wa polisi amewataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kuweza kuboresha zawadi zilizopo hali itakayoleta hamasa katika mashindano hayo nakuhahidi kuwepo kwa mashindano mengine baada ya kumalizika haya ya POLISI JAMII tarehe 27 julai 2024.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai