Mashirika yasiyo ya kiserikali yametakiwa kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao kwa wote wamelenga kuwahudumia wananchi.
Wito huo umetolewa na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Devid Lekei wakati wa kikao cha mashirika binafsi kilicho andaliwa na divisheni ya Maendeleo ya Jamii kwa lengo la kujadili fursa na changomoto zinazokabili mashirika hayo.
Lekei amesema serikali inatambua mchango wa taasisi binafsi katika kusaidia jamii na ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,na hivyo wakishirikana watawezesha ufikishaji wa huduma mbali mbali kwa wananchi.
Aidha alikemea baadhi ya mashirika yanayogomba na kusababisha migogoro katika taasisi hizo na jamii kwa ujumla.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai