Mashirika binafsi na yasiyoyakiserikali (NGO’S) yaliyopo wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro yameaswa kufanya kazi kwa weledi na kushirikiana kwa pamoja ili kuongeza tija katika utendaji kazi na kulinda maadili ya nchi pamoja na matumizi sahihi ya fedha za wadau wanaowekeza katika mashirika hayo.
Hayo yamesemwa na mwakilishi wa mashirika hayo wilaya ya Hai na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Hai Bi Happyness Eliufoo wakati akiongea katika mkutano wa mashirik hayo uliofanyika August 17,2024 katika ukumbi wa halmashauri ya (W) Hai, ambapo pia ameyataka mashirika binafsi kuwa na unawezo wakutumia fedha na kufanya kazi na wadau wa fedha katika mashirika yasiyoyakiserikali.
Katika kikao hicho kimeazimia mambo mbalimbali ikiwa nikuinua vikundi mbalimbali hasa wanawake kwa lengo lakutoa Elimu juu ya mambo muhimu katika maisha yabinadamu ikiwemo elimu kuhusu NSSF na mikopo kutoka CRDB kwenda vikundi mbalimbali sio tu kwa wafanyakazi bali hadi kaya masikini.
Vilevile kwa upande wake mwakilishi wa Makongo (W) Hai ambaye ni daktari bingwa wa macho na sayansi ya uzazi ameyaasa mashirika kutoa mikataba kwa wafanyakazi wa mashirika yao ili kulinda haki msingi za wafanyakazi wa mashirika yao, ameongeza kwakutoa wito kwa mashirika kuhakikisha ustaidi na weledi wa utendaji kazi pamoja nakulipa kwa mujibu wa mikataba.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai