Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Hai Yohana Sintoo amewataka mawakala wa vyama vya siasa watakaoshiriki zoezi la uchaguzi wa madiwani utakaofanyika tarehe 16 mwezi huu katika kata za Machame Uroki na Kia.
Sintoo ametoa rai hiyo wakati wa kuwaapisha mawakala hao kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Amewasisitizia kuwa waadilifu wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuepuka kuingilia majukumu yasiyowahusu kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria na taratibu za uchaguzi.
“Mmeapishwa leo kwa majukumu yenu kama wakala wa vyama vyenu, mtakutana na msimamizi mkuu, msimamizi msaidizi, pamoja na askari watakaoweka ulinzi kwenye vituo mtakavyokwenda; msiingilie majukumu yao” Amesema Sintoo.
Kwa upande wao mawakala walioapishwa wameahidi kutumia nafasi zao kutenda haki katika kutekeleza majukumu yao.
Uchaguzi mdogo wa marudio umepangwa kufanyika katika kata mbili za Machame Uroki na Kia ili kujaza nafasi wazi baada ya madiwani wa kata hizo kujiudhuru nafasi zao na kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai