Mbunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Mhe. Saashisha Mafuwe amezipongeza shule za taasisi ya kiislamu ya Mudio (Mudio Islamic Seminary) kwa kuendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Saashisha ametoa pongezi hizo leo Macih 4, 2021 alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwapongeza watendaji wa taasisi hiyo kwa lengo la kutambua mchango wao uliopelekea kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya kidato cha nne, kidato cha pili, darasa la saba na darasa la nne iliyofanyika mwaka jana 2020.
"Nawapongeza sana kwani mnafanya kazi ya kutupa heshima katika wilaya ya Hai na mkoa wa Kilimanjaro kwa hiyo mnapokaa na watoto hawa muwafundishe kuwa wabunifu na kuweza kujitegemea" amesema Saashisha.
Aidha mbunge huyo ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa vijana wanaomaliza kwenye taasisi ya Mudio kuwa chachu ya mabadiliko kwenye jamii kutokana na elimu waliyoipata kwenye taasisi hiyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Uongozi wa vituo vya Islamic Solidarity Mwl. Athuman Mtavangu ameiomba serikali kuweka utaratibu wa kupeleka walimu katika shule za Seminary ikiwemo ya Mudio kwa lengo la kuwatambua kufuatia huduma wanazozitoa kwa jamii.
Naye naibu ofisa mhubiri wa mkoa wa Kilimanjaro Alhaji Shekhe Dhahabu ambaye amemwakilisha Shekhe wa mkoa ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa jamii kutokuwa na hofu wala kutishana juu ya janga lililoikumba dunia huku akisisitiza kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.
Mudio Islamic Solidarity Center imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2020 ambapo kwa darasa la 4 imeshika nafasi ya 5 kimkoa huku darasa la 7 ikishika nafasi ya 7 kimkoa na kuongoza katika wilaya ya Hai.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai