Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kumalizia miradi mbali mbali ya maendeleo katika Jimbo la Hai.
Saashisha amesema kuwa lengo la kukabidhi vifaa ivyo ni kukamilisha miradi hiyo ikiwemo vyumba vya madarasa katika kata saba za wilaya ya hai pamoja na mifereji ya umwagiliaji iliyoharibiwa wakati wa mafuriko.
Amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia kwa uadilifu na kufuata taratibu, sharia na kanuni za usimamiri wa miradi ya serikali ili thamani ya fedha iendane na miradi husika.
Nae katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai Kumotola Laurance Kumotola amesema chama hicho hakitamwonea haya atakayeshindwa kusimamia matumizi sahihi ya fedha na vifaa vinavyotolewa na serikali au michango ya wananchi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Secondary Lerai iliyopo kata ya Bondeni ndugu Twaiba Nkya ambae ni miongoni shule zilizopata vifaa hivyo vya ujenzi ameshukuru kwa kupewa vifaa hivyo na kwamba vitapunguza upungufu wa vyumba vya madarasa kwani shule hiyo una uhitaji wa vyumba nane vya madarasa.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai