Mbunge wa Kundi la Wafanyakazi Mhe. Dkt Alice Kaijage amewataka Watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii wakati serikali inaendelea kutatua changamoto zao.
Akizungumza katika kikao kilicholenga kupokea changamoto zinazowakabili watumishi, Mhe Kaijage amesema serikali ya awamu ya Sita imeendelea kutatua changamoto za watumishi ikiwa ni pamoja na upandishwaji wa madaraja ambapo watumishi zaidi ya 400,000 tayari wamepandishwa.
Amesema Kama Mbunge wa Kundi la Wafanyakazi anatambua kuwa watumishi wana changamoto mbalimbali ndio sababu ya yeye kukutana na watumishi ili kuzipokea na kuzipeleka Mbungeni.
"Ni kweli bado Kuna changamoto,Kama mlivyo omba nizichukue, suala la Bima ya Afya, Muundo, pamoja na madai ya watumishi,ila lazima tumshukuru pia Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya dhati ya kutatua changamoto za watumishi mfano ,upandishwaji wa madaraja na malipo ya malimbikizo ya watumishi ambayo amefanyia kazi Kwa kiwango kikubwa"
Naye Mbunge wa Jimbo la Hai Saashisha Mafue amemshukuru Rais kwa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ii kiwa ni pamoja na Zaidi ya shilingi bilioni 2.8 zilizopokelewa hivi karibuni Kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali.
"Hawa watumishi unao waona ndio wanao simamia utekelezaji wa miradi katika wilaya yetu,ndio wanaotoa huduma muhimu zinazotolewa Kwa wananchi na wanafanya vizuri kweli kweli" Amesema Mafue.
"Tafadhali naomba nisaidie kuzipokea changamoto zao zote pamoja na zile nilizokupa uzifanyie kazi "alisisitiza Mafue
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai