Imeelezwa kuwa kesi nyingi za ukatili wa kijinsia zinazopelekwa mahakamani zinakosa ushahidi kutokana na mila potofu zinazoendelea katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Hai, Helga Simon wakati wa mahojinao na kituo cha boma hai fm na kusema kwamba matukio mengi ya ukatili yamekuwa yakisuluhishwa kifamilia na hivyo kufanya kesi nyingi kukosa ushahidi wanapofika mahakamani.
"Mila zinachangia Sana katika kushindwa kudhibiti watuhumiwa na kushindwa kumsaidia mhanga aliyeathiriwa na ukatili huo,matukio mengi yanasuluhishwa kijamii hivyo Kuna wimbi kubwa la watoto kufanyiwa ukatili na kesi nyingi mahakamani kupotea kwa kukosekana kwa ushahidi jambo linalosababisha muhathirika kukosa haki."amesisitiza Simon.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii Ester Msoka amesema idadi ya matukio yanayoripotia inazidi kuongezeka kutokana na elimu inayoendelea kutolewa na kuitaka jamii kuacha kusuluhisha matukio hayo ngazi ya familia badala yake watoe ushirikiano kwa mahakama na mamlaka zote zinazohusika.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai