Serikali inakamilisha utaratibu wa kutoa kiasi cha shilingi milini 500 kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili kwa kituo cha Afya Nkwasira na Masama kati wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Akijubu swali la Mbunge wa Hai Saashisha Mafue alilouliza leo tarehe 27/08/2024 katika kikao cha bunge akitaka kujua ni lini serikali itatao fedha kwa ajili ya ukamilshaji wa ujenzi wa vituo hivyo vya afya.
Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt Festo Dugange amesema kuwa serikali inatambua kuwa ilitoa fedha kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa vituo hivyo na kwa sasa ipo katika hatua ya mwisho kukamilisha malipo ya awamu ya pili ambapo kila kituo kitapata kiasi cha shilingi milioni 250.
"mhe.Spika serikali inatambua kwamba kituo cha afya cha Nkwansira na Masama Kati katika jimbo la Hai vilipewa fedha awamu ya kwanza milioni 250 na mhe.Mbunge amefuatilia sana, nikuhakikishie tupo katika hatua za mwisho za kupeleka fedha hiyo miloni 500 katika vituo hivyo viwili milioni 250 kwa kila kituo"
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai