Mwenge wa Uhuru kutembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi saba ya maendelo yenye thamani ya zaidi ya shilingi 1628 wilayani Hai.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kisare M. Makori ,Mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja uwekaji wa jiwe la msingi katika Zahanati ya Shirinjoro iliyojengwa kwa mapato ya ndani kiasi cha shilingi 88,000,000.
Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya Nyerere yenye urefu wa 0.79 kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi 429,323,755, mradi huo utawekwa jiwe la msingi na kuzindua ujenzi wa tanki la maji eneo la Kilimambogogo, kata ya Bondeni lililojengwa kwa shilingi 100,000,000 linalotarajiwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi 9500.
Mkalipa alitaja miradi itakayotembelea na kukaguliwa kuwa ni pamoja na mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji Njoro ya Blue wenye thamani ya shilingi 15,880,000 katika Kata ya Masama Rundugai na mradi wa uoteshaji wa mbogamboga na matunda kikundi cha Youth Greena Movement wenye thamani ya shilingi 31,000,000 katika kata ya Bondeni.
Aliendelea kutaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa majengo manne na nia za wagonjwa Hospitali ya wilaya ya Hai iliyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 900 na ujenzi wa vyumba vitatu vya sekondari katika shule ya sekondari Hai kwa gharama ya shilingi 64285,000
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai