Mkuu wa wilaya ya Hai mheshimiwa Amir Mkalipa amewataka viongozi wa dini kuwafundisha waumini kuwa na hofu ya Mungu kwa kutenda matendo mema na kuachana na maovu ili taifa liweze kuondokana na majanga mbalimbali.
Amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa dini na waumini wa madhehebu mbalimbali wakati akifungua maombi ya kuombea wilaya na taifa yalitofanyika katika viwanja vya halmashauri.
Ameongeza kuwa hofu ya Mungu inapokosekana katika jamii husababisha maovu kutokea na kufanyika katika jamii hivyo Kila mwananchi anatakiwa kuhudhurua katika nyumba za ibada ili kupata mafundisho yatakayowawezesha kuondokana na maovu na kutenda mema.
Ameongeza kuwa wazazi pia wana jukumu la kuwalea watoto katika maadili mazuri kwa kuwafundisha watoto kufanya kazi kwa bidii badala ya kuwaachia wasaidizi wa ndani kazi zote za nyumbani .
Akizungumzia kuhusu manyanyaso wanayopitia baadhi ya wafanyakazi wa ndani ,mkuu wa wilaya amewaasa wazazi na waajiri wanaowanyanyasa wasichana wa kazi kuacha mara moja tabia hiyo kwani atakayebainika hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake.
Nao baadhi ya viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali walioshiriki katika maombi hayo wamesema kuwa majanga yanayotokea katika jamii ni kutokana na uovu unaofanywa katika jamii hivyo jamii inapaswa kuomba rehema kwa Mungu na kuacha maovu
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai