Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Hai ameipongeza Idara ya Afya kwa kusimamia vema watoa huduma katika Wilaya hiyo hali iliyosababisha Wilaya kufanya vizuri katika tathmini ya ubora wa huduma inayofanywa na wizara ya afya kupitia mpango wa matokeao makubwa sasa iliyofanywa na Wizara ya Afya kwa mwaka huu ambapo Wilaya ya Hai imepata alama sitini na mbilii (62) na kushika nafasi ya pili Kimkoa ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2016 iliyokuwa na alama tano (5).
Amesema mabadiliko hayo yamewekezana kutokana na usimamizi dhabiti na ushirikiano ulipo kati ya Idara hiyo na vituo vyote vya Afya kwa kuwa tathimini hiyo ufanywa kwenye vituo na hosptali zote za binafsi, taasisi za dini na za serikali na kuitaka Idara hiyo kuendelea kusimamia vituo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwapa miongozo mbali mbali ya Serikali kwa wakati inapotokea mabadiliko.
Mkurugenzi ametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha kuiaga bodi ya Afya Wilaya kilichofanyika jana ambapo pia ameitaka idara hiyo kuweka mkakati wa kutoa elimu kwa jamii juu ya lishe na mfumo wa ulaji bora kwa jamii kupitia vyombo vya habari na mikutano mbali mbali ya kijamii ili kuboresha afya za wananchi na kuipunguzia serikali gharama inayotumika kugharamia magonjwa ambayo yanasababishwa mfumo mbovu wa leshe na wananchi kutofanya mazoezi.
‘Ni kweli tumetoka asilimia tano kwenda asilimi sitini na mbili,tusiishie hapa tuendelee kufanyia kazi maeneo ambayo yamekuwa na changamoto zilizojitokeza ili kwenye tathimini inayofuta tufanye vizuri zaidi, kwa vile vituo kumi bora vya wilaya vipewe vyeti na Wilaya hii ni motisha kwa vituo hivi vilivyofanya vizuri na itaamusha hari kwa vile vituo ambavyo havikufanya vizuri kwa kipindi hiki ,lakini pia tuweke bidii na uwajibikaji zaidi kwa dhamana kubwa ya kuokoa maisha ya wananchi wetu.’alisisitiza Sintoo.
Akisoma taarifa ya matokeo ya tathimini ya Ubora, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Hai dkt Irine Haule alisema matokeo hayo yamepatikana baada ya kupitia vituo vyote 61 vya kutolea huduma vilivyopo wilayani hai, na kwamba tayari wameweka mikakati ya kutatua baadhi ya changamoto zilizojitokeza ikiwa ni pamoja na uchakavu wa miundo mbinu,uhaba wa wataalam wa maabara,kukosekana na dawa muhimu ya dharura na kukosa miundo mbinu ya watu wenye ulemavu na kwamba tayari baadhi ya changamoto hizo zitafanyiwa kazi kupitia utekelezaji wa bajeti 2018/2019.
Dkt Haule amewashukuru wadau na wajumbe wa bodi ya afya kiwilaya kwa jitihada zao katika kuboresha na kusaidia mafanikio kupatikana na kuahidi kushirikiana na wadau wote hasa wamiliki wa vituo vya afya vya taasisi za dini na binafsi ili kuendelea kufanya kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi aliyemaliza muda wake ndugu Invocativith Swai amesema bodi hiyo inayomaliza muda wake imeweza kusimamia ukarabati wa vituo vitatu vya afya ,kuanzishwa kwa duka la dawa katika hospitali ya wilaya ,ukamilishaji wa wodi ya wananwake pamoja na kuhakikisha upatikanajia wa vifaa tiba, dawa na vitendanishi katika vituo vyote vya kutolewa huduma kwa asilimia Zaidi ya 80 na ununuzi wa jenereta hali ambayo imesadia kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Naye dkt Grace kutoka Moshi Specialist akielezea siri ya mafanikio ya kituo hicho kuwa kushika nafasia ya kwanza kiwilaya na nafasi ya pili kimkoa ni ushirikiano na umoja katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na ushirikiano mkubwa kutoka kwenye uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kutokana na usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara uliofanywa na timu ya wataalam kutoka Idara ya afya.
Katika matokeo hayo Halmashauri ya Hai imefanikiwa kutoa vituo vya Afya vitatu ambavyo vimafanikiwa kuingia kwenye kumi bora Kimkoa ,vituo hivyo ni Hospitali ya Wilaya ya Hai,kituo cha Afya cha Kisiki pamoja na Moshi Specialist.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai