Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai Yohana Sintoo ameagiza uongozi wa Redio Boma Hai kutumia redio hiyo kuwafahamisha wananchi mambo yanayotekelezwa na serikali katika maeneo yao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mdahalo ulioandaliwa na kituo hicho cha redio wakati wa maadhimisho ya siku ya redio duniani; Sintoo amesema kuwa uwepo wa redio kwenye wilaya ni faida kubwa ikiwa itatumika ipasavyo.
“Tengenezeni vipindi vya kuelezea mambo yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ili wananchi wafahamu namna serikali yao inavyowahudumia na kuachana na taarifa potofu wanazozipata mitaani”
Amepongeza namna redio hiyo inavyotoa huduma kwa jamii kwa kufanya vipindi vinavyoendana na mahitaji halisi ya jamii ya watu wa Wilaya ya Hai.
Awali akichangia kwenye mdahalo huo; katibu wa CCM Wilaya ya Hai Kumotola Kumotola amewataka wataalamu wa Halmashauri wakiongozwa na wakuu wa Idara kutumia redio kuelezea utekelezaji wa kazi unaofanyika kwenye idara zao ili jamii ielewa mambo yanayotendeka hasa katika utekelezaji wa Ilani ya CCM kama chama kinachounda serikali.
Naye Afisa Habari Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa mdahalo huo; Shaban Pazi ameitaka jamii kutumia vizuri maudhui yanayotangazwa na redio katika vipindi mbalimbali vya kuelimisha ili kubadilisha maisha yao huku akiwakumbusha wanahabari kutumia taaluma yao kuandaa maudhui kulingana na mahitaji ya jamii wanayoihudumia.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai