Maafisa waandikishaji wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufanya Kazi hiyo kwa haki, weledi na kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Hayo yamebainishwa hii leo na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Yohana Sintoo wakati akifungua semina kwa waandikishaji hao wapatao 314 iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo huku ikiambatana na kiapo cha uaminifu.
Sintoo amesema kutokana na uchaguzi huo kuwa wamuhimu zaidi katika TAIFA Ni vyema sasa maafisa hao wakaelewa wajibu wao wa kusimamia uchaguzi huo kisheria na kuhakikisha kila mwananchi Mwenye sifa anapata nafasi yakujiandikisha bila kikwazo cha aina yoyote huku akiahidi kufuatili kwa umakini utekelezaji wa zoezi hilo.
Kwa upande wake Hakimu mkazi wilaya ya Hai Lazaro Benedict Kadendula amewataka maafisa hao kutunza siri ya utendaji Kazi pamoja na kufanya zoezi hilo kwakuzingatia kiapo walichokiapa kwa mujibu wa katiba na sheria ya uchaguzi na kwamba kwenda kinyume watashitakiwa kulingana na kiapo walichokiapa.
Nae Msimamizi wa uchaguzi huo Jimbo la Hai Bw. Juma Masatu amewataka kuwa na misingi mizuri na Ushirikiano ili kuweza kufanikisha zoezi hilo kwa wakati uliopangwa huku akisistiza kuwa jimbo la Hai limesha limeshajipanga kuhakikisha uandikishwaji pamoja na Uchaguzi unafanyika katika Mazingira ya jamani na haki.
Zoezi la Uandikishaji litaanza kote nchini Jumanne ya tarehe 8 hadi tarehe 14 mwezi oktoba huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika tarehe 24 mwezi novemba mwaka huu na Uchaguzi huo unaongozwa kwa kanuni za uchaguzi wa viongozi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa katika mamlaka za Wilaya na mamlaka za Miji, kwa mujibu wa matangazo ya Serikali Na. 371, 372 373 na 374 ya mwaka 2019.
Kitongoji cha Bomani
Anuani ya Posta: 3 RD TTCL RC CHURCH 25382, P.O BOX 27 Hai
Simu: 0754553560
Simu ya Mkononi: 0754553560
Barua Pepe: ded@haidc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Hai